Alhamisi 11 Juni 2026 - 13:15
Wananchi wa Lebanon Wakusanyika Mbele ya Ubalozi wa Iran, kama Ishara ya Uaminifu na Shukrani kwa Kusimama Iran Pamoja na Lebanon

Hawza/ Wananchi wa Lebanon walikusanyika mbele ya Ubalozi wa Iran mjini Beirut kama ishara ya kutoa shukrani kwa hatua ya Iran ya kujibu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na kuiunga mkono Lebanon.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kama ishara ya uaminifu kwa taifa kubwa la Iran ambalo halijawahi kusita kusimama pamoja na Lebanon katika nyakati ngumu zaidi, na kama jibu kwa msimamo thabiti wa Iran kwamba: “Hatutaiwacha Lebanon peke yake,” makumi ya watu huru na wenye heshima walikusanyika jioni ya leo Jumanne mbele ya Ubalozi wa Iran mjini Beirut.

Mkusanyiko huu ulikuwa ni uthibitisho kwamba; malipo ya heshima ni heshima, na malipo ya uaminifu ni uaminifu; na kwamba mataifa yaliyo hai hayawasahau wale waliosimama pamoja nao katika nyakati za mitihani na matatizo.

Wananchi wa Lebanon Wakusanyika Mbele ya Ubalozi wa Iran, kama Ishara ya Uaminifu na Shukrani kwa Kusimama Iran Pamoja na Lebanon

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha